VALENTINE POEM: CHAGUO LANGU

1
116

Mapenzi sio ya nguo, kila mtu kumiliki
Wewe ndo langu chaguo, moyo umekuafiki
Pia kwako ni funguo, juu yako ninaloki
Hata aje mwenye cheo, upendo wetu haufi.

Nakupenda bila kituo, kwa raha hata kwa dhiki
We bahari mi ufuo, hakika shaweka tiki
Tena bila kipumuo, sipotezi zo ashiki
Hata aje mwenye cheo, upendo wetu haufi

Nakupenda mahabuba, penzi liso na kifani
Nd’oo tupeane huba, dhahiri so faraghani
Nalienzi lako huba, kulikosa sitamani
Hata aje mwenye cheo, upendo wetu haufi

Sisikize ya fulani, penzi letu taharibu
Leo siku yetu hini, takulisheni zabibu
Sitokwacha asilani, ‘kakutieni aibu
Hata aje mwenye cheo, upendo wetu haufi

Ewe wangu wa ubani, nikuenziye moyoni
Japo nakutamani, Kwa huba ziso kifani
Tailinda turuhani, uwe wangu maishani
Hata aje mwenye cheo, upendo wetu haufi

Kalamu naweka chini, Kwa raha na Kwa bashasha
Nenda tulia kochini, tena bila mshawasha
Kwaheri nakuageni, singependa kukuchosha
Hata aje mwenye cheo, upendo wetu haufi.

See Also:  9 Feared Dead After a Mombasa Bound Bus Collides With Lorry.

For more contact Demalix# FB

Or 0702 856799

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here